Top Stories

MAHAKAMANI: Ilivyokuwa kuwa kesi ya Sugu leo na ishu ya dhamana yake

on

Leo January 19, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imeamuru Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kurudishwa mahabusu mpaka Jumatatu ya January 22, 2018 kesi yake pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini  Emmanuel Masonga itakapoanza kusikilizwa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Michael Mteite ametoa uamuzi huo leo huku akitoa sababu kuwa kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi na washtakiwa wakiwa wanafika Mahakamani wakitokea mahabusu.

“Mahakama inataka kusikiliza kesi kwa muda mfupi, ndani ya wiki moja kuanzia Jumatatu iwe imeamuriwa, hivyo washtakiwa wataendelea kuwekwa mahabusu,” Hakimu Mteite

Mbilinyi na Masonga wameshtakiwa kwa kosa la kumfedhehesha Rais JPM ambayo walitoa katika mkutano wa hadhara walioufanya December 30, 2017 wakiwa viwanja vya shule ya msingi Mwenge jijini Mbeya.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili. Wakili anayewatetea Sabina Yongo ameiomba Mahakama kuyapitia mashtaka ya wateja wake na kuomba Mahakama itoe dhamana.

Hata hivyo Wakili wa Serikali Joseph Pande ameiomba Mahakama kufunga dhamana kwa usalama wa watuhumiwa.

Akisoma uamuzi wa Mahakama Mteite amesema washtakiwa watarudi Mahabusu hadi January 22, 2018 kesi hiyo itaposikilizwa na upande wa mashtaka watakapotoa ushahidi na siku inayofuata washtakiwa watajitetea na hukumu kutolewa ndani ya wiki hiyo. 

GARI YA FFU IMEPINDUKA KUTOKANA NA MWENDOKASI IMEUA ASKARI 2, KAMANDA MPINGA KAONGEA

Soma na hizi

Tupia Comments