Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Saudi Arabia kuhusu Nishati Safi ya Kupikia.
Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika Dar es Salaam Ujumbe huo uliambatana pia na Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya bin Ahmed Okeish, Meneja wa Mpango wa Nishati Safi ya Kupikia Bi. Reema Al Ashgar na Mhandisi wa mradi Bw. Faisal Al Mahsn wote kutoka Wizara ya Nishati ya Saudia.
Waziri Masauni amesema ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia baada ya Jumuiya za Kimataifa kuanzisha kampeni hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa wa kwanza kuibeba na kuileta nchini Tanzania kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo jambo ambalo limeongeza msukumo na kukuza matumizi ya nishati safi hasa katika maeneo ya vijijini.
“Ofisi ya Makamu wa Rais moja ya eneo ambalo inasimamia ni Uhifadhi na Utunzajii wa Mazingira hivyo Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika eneo hili inasaidia kwa kiwango kikubwa katika kutunza mazingira.
“Tunashukuru kwa kuiona Tanzania moja ya nchi ambayo imekuwa kinara katika uhamaishaji wa matumiazi wa nshati safi ya kupikia hivyo niseme kwamba milango ipo wazi katika kuunga mkono jitahada hizi zinazofanywa na viongozi mbalimbali,” amesema Waziri Masauni.
Ameomengeza kuwa matumizi ya nishati chafu sio tu inaharibu mazingira bali hata afya za binadamu ambao hutumia kwa kuwa moshi wa kuni huwa na sumu ambayo humuathiri mtumiaji ndio maana serikali hufanya jitihada mbalimbali katika kulinda wananchi wake.
Katika hatua nyingi Mhe. Waziri emesema Tanzania pia imekuwa ikipiga hatua katika Biashara ya Kaboni kupitia Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kilichopo mkoani Morogoro hiyo yote ni katika jitihada za kulinda na kutunza mazingira na milango ipo wazi kwa wote wenye nia ya kuwekeza eneo hilo.