Top Stories

Mabadiliko makubwa 10 aliyofanya Rais Magufuli kwa Ma-RC na Ma-DC leo

on

Leo July 28, 2018 Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa, wa Wilaya na Makatibu Tawala nchini huku akiwateua wanasiasa watatu waliowahi kuwa vyama vya upinzani katika nafasi hizo.

Rais John Pombe Magufuli amemteua Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Hapi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.


Rais John Pombe Magufuli amemteua Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Katambi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA)


Rais John Pombe Magufuli amemteua Lengay Ole Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Kilimanjaro.

Rais John Pombe Magufuli amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Kafulila aliwahi kuwa Mbunge kupitia chama cha NCCR-Mageuzi.


Rais John Pombe Magufuli amemtua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Pwani, Jokate aliwahi kuwa Katibu wa Uenezi wa UVCCM.


Rais John Pombe Magufuli amemteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Arusha, Jerry aliwahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga.

Rais Magufuli amemhamisha Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na kumpeleka Mkoa wa Katavi.

BREAKING: JPM ATANGAZA MABADILIKO WAKUU WA MIKOA/WILAYA… JOKATE, JERRY MURO WAULA

Soma na hizi

Tupia Comments