Leo July 19, 2018 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Athuman Kihamia amezungumza na AyoTV na millardayo.com kuhusu baadhi ya wagombea wa upinzani kunyang’anywa fomu wakati wanapozirudisha na wengine kupewa mitihani ya kuandika.
Kihamia akijibu tuhuma zilizowasilishwa na CHADEMA amesema sio kweli kwamba hajajibu barua za CHADEMA bali kuna utaratibu na kuna vikao.
“Kazi yangu sio kujibu kwenye mitandao NEC tuna utaratibu, barua ikija lazima tukae kwenye vikao vya Tume tuijadili, sio kila kitu katika uchaguzi kinajibiwa na Tume kama ni ugomvi huo ni wa Polisi, mpaka saivi hali inaenda vizuri” Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Kihamia
‘Huku ndiko Rais Magufuli anataka twende’ – Mbunge Seif Gulamali