Top Stories

BREAKING: Msafara wa Rais Magufuli umepata ajali

on

Leo September 4, 2018 Msafara wa Rais John Magufuli umepata ajali katika kijiji cha Kasuguti Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara ikihusisha magari manne kugongana na kusababisha gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari kupinduka na kupelekea baadhi ya waandishi kuumia sehemu mbalimbali za miili yao. 

Wakati ajali hiyo ikitokea, gari za Rais Magufuli zilikuwa zimepita umbali mrefu kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo.

Taarifa za awali zinadai kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri. Taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitakujia hapahapa millardayo.com

“Umasikini hauna aibu utabaki uchi /ukae mguu pande mguu sawa”RAIS MAGUFULI

Soma na hizi

Tupia Comments