Simon Petrus Mwanafunzi wa Sekondari amegundua simu isiyotumia vocha wala kadi, kijana huyo raia wa Namibia ameuelezea ugunduzi wake kuwa unatumia mawimbi ya redio na hauhitaji kuwa na ‘simcard na airtime’.
Amesema kuwa imemchukua miaka 2 kukamilisha ugunduzi huo alioufanya kwa kutumia mabaki ya simu na runinga zilizoharibika.
Wazazi wake ambao hawana ajira kwa sasa walihangaika kumsaidia kijana wao ili akamilishe mradi huo uliogharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Nne.