Michezo

KAGAME CUP: Azam FC yaipiga TP Mazembe ya Katumbi

on

Mabingwa watetezi, Azam FC wamekuwa wa kwanza kutinga nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki yajulikanayo kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya T.P Mazembe ya DR Congo kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali Rwanda.

Haikuwa kazi nyepesi kwa Azam ililazimika kupigana haswa baada ya kutoka nyuma ili kupata tiketi hiyo, Mazembe walitangulia kufunga goli dakika ya 21 kupitia Ipamy Giovanni, huku Azam ikipiga mapigo na kusawazisha kupitia kwa Idd Suleiman dakika ya 27, huku Mzambia Obrey Chirwa akiimaliza bao la ushindi kwa Azam dakika ya 69.

Michezo mingine ya robo fainali itapigwa leo kati ya Gor Mahia ya Kenya itakutana na Green Eagles ya Zambia, huku wenyeji APR watavaana na AS Maniema ya DR Congo, washindi wawili wataungana na Azam FC katika nusu fainali.

TAZAMA BONGO ZOZO ANAVYOENDA UWANJANI MECHI YA TAIFA STARS NA KENYA

Soma na hizi

Tupia Comments