Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli leo August 1, 2018 amewaapisha Wakuu wa mikoa, Makatibu tawala, Makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara ambapo ametoa Maagizo mbalimbali baada ya kuwaapisha, hapa nakusogezea MAAGIZO KUMI.
Agizo la Kwanza alilotoa JPM ni “Kuna mkubwa mmoja alifanya mambo ya hovyo Wizarani, nikamuuliza Waziri kwanini usimtengue? akasema hana Mamlaka, nikampa DK 15 nikamwambia kasome Sheria ukikuta ni Mimi nina mamlaka namtengua nakutengua na wewe, ndani ya dakika tano akamtengua” Rais Magufuli
“Kuna mkubwa mmoja alifanya mambo ya hovyo Wizarani, nikamuuliza Waziri kwanini usimtengue? akasema hana Mamlaka, nikampa DK 15 nikamwambia kasome Sheria ukikuta ni Mimi nina mamlaka namtengua nakutengua na wewe, ndani ya dakika tano akamtengua” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/JrbFVyaJ7x
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Pili ni kuwa na ushirikiano “Unakuta RC hawaongei na RAS naomba mkashirikiane maana sisi tungekua hatuongei sidhani kama tungekuwa hapa hivyo mkajenge mahusiano na wale mnaowaongoza maana mmepewa majukumu makubwa na nchi hivyo mkayatumie vizuri” Rais Magufuli
“Unakuta RC hawaongei na RAS naomba mkashirikiane maana sisi tungekua hatuongei sidhani kama tungekuwa hapa hivyo mkajenge mahusiano na wale mnaowaongoza maana mmepewa majukumu makubwa na nchi hivyo mkayatumie vizuri” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/EZ8oafjLPG
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Tatu ni kuelewa majukumu yao “Mkienda huko mkafanye kazi, mawaziri mzielewe wizara zenu, kuna baadhi ya mawaziri hamzijui vizuri wizara zenu” Rais Magufuli
“Mkienda huko mkafanye kazi, mawaziri mzielewe wizara zenu, kuna baadhi ya mawaziri hamzijui vizuri wizara zenu” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/f6MywgyPN2
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Nne alilotoa JPM leo ni msisitizo suala la ukusanyaji mapato “Sasa mimi huku Rais nakazania mapato, wewe Rais wa mkoa umeshindwa kusimamia mapato sasa kwanini nisijiulize kwamba hufai” Rais Magufuli
“Sasa mimi huku Rais nakazania mapato, wewe Rais wa mkoa umeshindwa kusimamia mapato sasa kwanini nisijiulize kwamba hufai” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/367JESVJ8k
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Tano ni kuhakikisha wanatatua kero za wananchi “Utakuta hata machinga wanasimama barabarani hawana mahali pa kufanyia biashara, wakina mama wamezulumiwa lakini viongozi wapo, hivyo nataka niwaambie viongozi mlioteuliwa hakuna mwenye garantii ya kazi” Rais Magufuli
“Utakuta hata machinga wanasimama barabarani hawana mahali pa kufanyia biashara, wakina mama wamezulumiwa lakini viongozi wapo, hivyo nataka niwaambie viongozi mlioteuliwa hakuna mwenye garantii ya kazi” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/gy6OF3jWdu
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Sita kuhakikisha wanafanyakazi za Wananchi “Sisi wote Viongozi tutambue kwamba Mungu aliamua tukatumikie nafasi hizi kwa manufaa ya watanzania Milioni 55 na inabidi kuwatanguliza mbele watanzania kwanza” Rais Magufuli
“Sisi wote Viongozi tutambue kwamba Mungu aliamua tukatumikie nafasi hizi kwa manufaa ya watanzania Milioni 55 na inabidi kuwatanguliza mbele watanzania kwanza” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/y54lQHHj45
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Agizo la Saba amewaeleza kuwa kikubwa ni kuwajibika na hakuna anaestahili zaidi ya mwingine “Waziri Mkuu sijui nilimchaguaje, kuna watu walivaa suti wakaenda Dodoma wamejiandaa kuwa Mawaziri Wakuu lakini hawakuwa akawa Kassim Majaliwa lakini haina mana kwamba Majaliwa ndio muhimu na anastahili sana kuwa Waziri Mkuu” Rais Magufuli akiapisha Ikulu leo.
“Waziri Mkuu sijui nilimchaguaje, kuna watu walivaa suti wakaenda Dodoma wamejiandaa kuwa Mawaziri Wakuu lakini hawakuwa akawa Kassim Majaliwa lakini haina mana kwamba Majaliwa ndio muhimu na anastahili sana kuwa Waziri Mkuu” Rais Magufuli akiapisha Ikulu leo.#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/CSgJUmso5I
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Jambo la Nane JPM amewaeleza ilivyokuwa kazi ngumu kuwapata aliowateua “Kazi ya kuwapata nyinyi haikua rahisi nimekaa na majina yenu kwa miezi minne wapo waliopungua na wapo walioongezeka hivyo unaweza ukaona kutafuta kiongozi ni kazi ngumu” Rais Magufuli
“Kazi ya kuwapata nyinyi haikua rahisi nimekaa na majina yenu kwa miezi minne wapo waliopungua na wapo walioongezeka hivyo unaweza ukaona kutafuta kiongozi ni kazi ngumu” Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/rtOsCekE0C
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Jambo la Tisa ni kwa wanaosema ameteua wapinzani “Wapo niliowateua, wengine wakasema nimewachagua wa upinzani, hivi kuna mpinzani wa Tanzania? Mtu kama Kafulila huyu alieipigania sakata la IPTL utasema ni mpinzani? Huyu si mpinzani huyu alikuwa anatekeleza vilivyo ilani ya CCM” Rais Magufuli
“Wapo niliowateua, wengine wakasema nimewachagua wa upinzani, hivi kuna mpinzani wa Tanzania? Mtu kama Kafulila huyu alieipigania sakata la IPTL utasema ni mpinzani? Huyu si mpinzani huyu alikuwa anatekeleza vilivyo ilani ya CCM” Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/C1S9JDWdvg
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
Jambo la 10 na la mwisho ni mfano alioutoa kwa wanaombeza kuteua wapinzani “Hivi ndugu zangu ukiteka vifaru, bunduki, hivi utaziweka kwenye stoo au utazipeleka zikatumike kuwashambulia hao hao maadui? Pia ukiwateka Mabrigedia na Mameja utawaacha au uwapeleke kulekule wakawe chambo ya kufanya vita inoge na mshinde” Rais Magufuli
“Hivi ndugu zangu ukiteka vifaru, bunduki, hivi utaziweka kwenye stoo au utazipeleka zikatumike kuwashambulia hao hao maadui? Pia ukiwateka Mabrigedia na Mameja utawaacha au uwapeleke kulekule wakawe chambo ya kufanya vita inoge na mshinde” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/btHpb2mmW3
— millardayo (@millardayo_) August 1, 2018
RC Mpya Iringa Ally Hapi alivyoapishwa na Rais Magufuli Ikulu