Top Stories

BREAKING: Hans Pope Simba anatafutwa na TAKUKURU, donge nono limetangazwa

on

Leo September 14, 2018 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa {TAKUKURU} imemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope kujisalimisha katika ofisi zake au Kituo cha Polisi.

Mbali na Hans Pope, TAKUKURU imemtaka pia Frankline Lauwo kujisalimisha, huku wote wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili juu ya mashtaka ya kutoa taarifa za uongo TRA.

TAKUKURU imetangaza zawadi nono kwa Mwananchi yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Watuhumiwa hao baada ya kutafutwa bila mafanikio.

SURPRISE: Bondia Wakinyo alivyotinga Bungeni, Spika “mshikeni mpaka kwa Waziri Mkuu”

 

Soma na hizi

Tupia Comments