Top Stories

BREAKING: Watu 7 wafariki gari la CAG na la PSSSF yakigongana uso kwa uso

on

Watu saba waliokuwa wakisafiri katika gari lenye namba za usajili STL 6250 mali ya CAG wamefariki papo hapo na wengine wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari lenye namba SU 41173 mali ya PSSSF, katika eneo la Chalinze Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma leo.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na inasemekana Watu waliofariki katika ajali ya gari hiyo ni dereva wa ofisi CAG na wengine 6 ni ndugu wa Naibu CAG waliokuwa wakitoka katika msiba Chato mkoani Geita.

“Sita waliofariki wapo Hospitali ya Kongwa, Dereva yupo Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, kulikuwa na gari imeharibika barabarani aina Leyland, hii STL iligonga nyuma kabla ya kugongana uso kwa uso na ya PSSSF ila tunaendelea na uchunguzi” Muroto

Ukweli kuhusu Balozi wa Umoja wa Ulaya kudaiwa kufukuzwa Tanzania

 

Soma na hizi

Tupia Comments