Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Diwani Athumani ameongea na Vyombo vya habari akiwataka wananchi kuongeza kasi kusoma alama za nyakati maana serikali ya awamu hii sio salama kwa wala Rushwa.
Akiwa Mkoani Kagera CP Diwani amesema kuwa TAKUKURU inayoongozwa na yeye itatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia Sheria haitaangalia itikadi, hadhi au cheo ulichonacho, atakayejihusisha na vitendo vya Rushwa hatabaki salama.