Top Stories

“Nampa siku 14 IGP, nataka aniambie wamesalimu amri?” – Kangi Lugola (+video)

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Kangi Lugola amempa siku 14 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro kumueleza mikakati ya kuwawezesha Watanzania kufanya kazi kwa saa 24 ikiwa ni pamoja mabasi kutembea nyakati za usiku.

Waziri Lugola ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo Ukonga na kuongea na Askari wa Kikosi hicho.

“Nataka IGP aje aniambie kwamba je? Jeshi la polisi limesalimu amri kwa majambazi ndio maana mabasi hayatembei usiku? lakini biashara mbalimbali ikifika saa 12 zinafungwa, ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya usalama, nataka IGP aniambie kama majambazi ndio wanaotupatia amri” alisema Kangi Lugola

“Hatuwezi kukubali kupewa amri na majambazi ni masaa mangapi tunatakiwa kufanya shughuli za kiuchumi au kupangiwa maeneo ya kwenda na wapi tusiende” akaongeza kwa kusema Waziri Lugola.. mtazame alivyotoa hili agizo kwenye hii video hapa chini

VIDEO: MUME KAENDA KAZINI, WIFE KALETA MCHEPUKO NYUMBANI… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

UMEPITWA? HAYA NI MAJIBU YA LAZARO NYALANDU BAADA YA KUAMBIWA ARUDISHE TWIGA

Soma na hizi

Tupia Comments