Top Stories

Rais Magufuli “Lowassa washauri unaowaongoza la sivyo wataishia Gerezani” (+video)

on

Rais Magufuli amempongeza Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kwa kuhudhuria  shughuli ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha DSM, akisema kuwa kitendo hicho ni cha kiungwana.

JPM  “Siku zote huwa nasema, Lowassa umekomaa kisiasa, ndio maana unahudhuria katika shughuli za kimaendeleo, maendeleo hayana, chama, kabila, dini, wala rangi,” 

“Nakupongeza sana Lowassa kwa utulivu wako, Wewe ndo tuligombea Urais lakini nilipokutupa chini ukaenda ukapumzika Mzee wa watu wenye kelele wengine hata hawakugombea, Wewe unajua ktk mashindano yoyote kuna kushindwa” -Rais Magufuli

“Vyama vyetu kamwe visiwe chanzo cha kututenganisha, nimeona nizungumze kwa heshima kubwa Mzee Lowassa ili wale unaowaongoza kule angalau ukawashauri otherwise wataishia kwenye Magereza”,- Rais Magufuli

LIVE : Rais Magufuli kwenye Ufunguzi wa Maktaba ya kisasa UDSM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

 

Soma na hizi

Tupia Comments