Top Stories

Waliosafirisha kobe 201 waamriwa kulipa Milioni 40

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu wanne waliojihusisha na usafirishaji wa Kobe 201 wenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 30 kulipa fidia ya Sh.Mil 40 baada ya kupatikana na hatia katika kesi hiyo.

Washtakiwa hao ni David Mudi mkazi wa Ilala Mohamed Salum Mohamed, Mustapha Bakari, Salum Wakili na Shabani Haji wote ni wakazi wa Nzanzibar.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Janet Mtega ambapo amesema washtakiwa hao wanahukumiwa kulipa fidia ya Sh.Mil 40 kwa utaratibu uliooneshwa katika hati ya makubaliano.

Washtakiwa hao ni miongoni mwa washtakiwa waliomwandikia barua ya kukiri na kuomba msamaha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na kosa moja ambapo wanadaiwa kati ya Novemba mosi hadi 16 mwaka 2015, kati ya maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam, wote walijihusisha na usafirishaji wa Kobe 201 wenye thamani ya milioni 30 milioni bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyamapori.

MTOTO MDOGO ALIVYOMFURAHISHA MAGUFULI, AMPA USHAURI JUU YA WANAUME

Soma na hizi

Tupia Comments