Top Stories

BREAKING: Waziri Lugola atoa kauli tukio la kutekwa Mo Dewji

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Jeshi la polisi linaendelea na mchakato wa kumtafuta mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji “Mo Dewji” aliyetekwa siku ya Alhamis Oktoba 11,2018 jijini DSM.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kangi amesema takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi ili kusaidia kutoa ushirikiano wakati wakiendelea kuwasaka watu wote waliohusika na tukio la utekaji ikiwemo kumpata Dewji mwenyewe.

”Niwahakikishie watanzania, jeshi la polisi linaendelea kushughulikia tukio la kutekwa kwa Mohamedi Dewji, likiwasaka waliomteka na tutahakikisha wanapatikana, ambapo hadi sasa navyozungumza takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano”, -Lugola

Lugola pia amemtaka IGP Simon Sirro kutoa maelekezo kwa askari wake, kuwaachia ndani ya saa 24 watu wanaowashikilia kwa uchunguzi kuhusiana na kutekwa kwa Mohammed Dewji mara baada ya kuwahoji na kubaini hawahusiki au hawana taarifa kamili.

LIVE MAGAZETI: Polisi wamsaka MO Dewji Bahari ya Hindi, Mkewe apewa ulinzi, CCM kuna majizi

Soma na hizi

Tupia Comments