Top Stories

Kamanda “tunamshikilia Dudu Baya anakera watu, anagusa hisia za watu” (+Audio)

on

Kamanda wa Polisi Kinondoni amesema wanamshikilia Msanii Godfrey Tumaini maarufu ‘Dudu Baya’ katika kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano. “Kuna malalamiko anarusha taarifa ambazo zinagusa hisia za watu juu ya Marehemu Ruge jamii inakerwa, tunafanya uchunguzi”.

Anatuhumiwa kumkashfu na kutoa lugha za kejeli kwa marehemu Ruge Mutahaba. Jana waziri wa habari, utamaduni na michezo Harrison Mwakyembe aliagiza Baraza la taifa la sanaa kwa kushirikiana na jeshi la polisi kumkamata msanii huyo kutokana na maneno ya dhihaka aliyozungumza mitandaoni kufuatia kifo cha Ruge.

WARAKA WA MAKAMBA: NISIKILIZE RUGE, SIJALIPA DENI, NIPE ISHARA

Soma na hizi

Tupia Comments