Top Stories

Watu wa Tanga wafunguka Mbakaji anaejipaka oil chafu, anatembea utupu (+video)

on

January 22, 2019 Wakazi wa Mtaa wa Gofu Juu Mtaa wa Mwamboni Kata ya Nguvumali Mkoani Tanga wamesema wanafanya jitihada za kumtafuta mtu mmoja anayefanya vitendo vya kihalifu nyakati za usiku.

Wakazi hao wamesema mara kwa mara mtu huyo mwenye jinsia ya kiume huvamia nyumba za wakazi wa eneo hilo kupitia juu ya dari na kisha kuiba simu na fedha na kuwabaka wanawake kisha kukimbia.

Joseph Asie ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Gofu juu amesema baadhi ya wananchi wake wamekuwa wakimletea malalamiko hayo na wengine wakithibitisha kufanyiwa vitendo hivyo vya ubakaji hivyo kutokana na taarifa hizo wameanzisha ulinzi shirikishi kwa ajili ya kumkamata kijana huyo.

DC MKOANI KWA MWANRI ATANGAZA MSAKO “HAIWEZEKANI MBINGUNI NA JEHANAMU”

Soma na hizi

Tupia Comments