Top Stories

Jamaa aliedharau agizo la Rais Magufuli kuhusu Korosho (+video)

on

November 12 2018 Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli alisema kuwa korosho zote nchini zitanunuliwa na serikali kwa bei ya shilingi 3300 kwa kilo moja jambo ambalo wakulima wa korosho wa mikoa ya kusini wamelipokea kwa furaha sana,

Leo Mtwara wilaya ya Newala kuna baadhi watu baada ya kuona bei ni kubwa ya korosho wameanza kuingiza korosho kutoka nchi jirani ya Msumbiji kimagendo kuja kuuza nchini.

AyoTV imepiga kambi katika wilaya ya Newala ambapo Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo amefanya msako mkali katika mipaka wa Tanzania na Msumbiji na kukuta mtu akiingiza gunia zaidi 90 zenye uzito wa kilo 100 kila moja.

Alivyojitetea jamaa aliedharau agizo la Rais Magufuli kuhusu korosho Mtwara

Soma na hizi

Tupia Comments