Top Stories

Zitto Kabwe amkaribisha January Makamba “tupambane”

on

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa Instagram kumkaribisha Mbunge mwenzake Makamba kukaribia tena ‘Backbench’ (nafasi za nyuma ndani bungeni) kuendelea na kazi ya Ubunge

Zitto katika ukurasa wake wa Instagram anaotumia jina la zittokabwe ameeleza baadhi ya sifa za mbunge huyo wa Bumbuli huku akiambatanisha na picha waliyokuwa pamoja nje ya Bunge la Tanzania.

“Rafiki yangu January Makamba karibu tena Backbench tuendelee na kazi. Ulikuwa Mbunge bora sana back bench 2010-2012 na ninaamini itakuwa hivyo tena 2019-2020.”

“Umekuwa mmoja wa mawaziri bora kabisa ambao umeonyesha tofauti ya kutawala na kuongoza. Namna ulivyoongoza marufuku ya mifuko ya plastiki ilionyesha falsafa yako ya uongozi ni tofauti sana na falsafa ya Serikali yenu ya CCM.”

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ameendelea kusema, “Tuna kesho nyingi tupambane kuijenga Tanzania inayojali watu wake na ya kidemokrasia.”

JIKO LINALOTUMIA SPIRIT “CHAI INAIVA DAKIKA MBILI”

Soma na hizi

Tupia Comments