Top Stories

DC Jokate atoa maagizo ya Rais Magufuli kwa Mgambo “mkapambane” (+video)

on

Leo November 27, 2018 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ametoa maagizo kwa Askari wa Jeshi la Akiba wanaohitimu mafunzo Wilayani humo kwenda kupambana na wanaohujumu Uchumi wa nchi kama ambavyo Rais Magufuli aliagiza akiwa Ikulu.

DC Jokate “Mkiweza kutambua Mtu anaehujumu Uchumi na mkitoa taarifa, jambo la Ulinzi na Usalama sio jambo la Viongozi peke yao, lazima Jamii ishiriki, tunategemea nyinyi kama Vijana mtumie hii fursa vizuri”

“Rais alishasema Hifadhi za Misitu ziheshimiwe na nadhani alitoa akiwa anaapisha Viongozi Ikulu kwamba Tanzania ni kati ya Nchi chache Duniani zenye eneo kubwa la Hifadhi, lazima Sisi tuliopewa dhamana kusimamia haya maeneo tuhakikishe misitu haiwezi kuingiliwa” -DC Jokate

DC JOKATE ASHUHUDIA MGAMBO WAKIRUSHIANA RISASI KISARAWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

JPM “LOWASSA WASHAURI UNAOWAONGOZA LA SIVYO WATAISHIA GEREZANI”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments