Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Wema Sepetu amekamatwa na Askari nje ya Mahakama

on

Leo July 4, 2019 Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu ameachiwa huru na kukamatwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wema ambaye aliwahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2006 anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Uamuzi wa Wema kuachiwa huru umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde chini ya kifungu cha 225(5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Awali Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda aliieleza mahakama kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili kusikilizwa lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea wamepewa taarifa kuwa anaumwa.

Hata Wakili wa Wema, Albert Msando amedai kuwa taarifa iliyotolewa mahakamani hapo haijajitosheleza huyo ameanza kuumwa jana au juzi hivyo walitakiwa kutoa taarifa zinazojitosheleza inapotokea pale shauri linataka kuahirishwa.

Pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa zinazojitosheleza nakumbuka mahakama ilitoa agizo kama inapotokea mtu anaumwa anatakiwa apeleke hati inayothibitisha ndio kutokana na hilo ilimsababishia Wema kuwekwa rumande kwa wiki moja iweje huyo shahidi asifanye kama mahakama inavyotaka,”amedai Msando.

Msando amedai mahakama hiyo ilitoa ahirisho la mwisho katika shauri lililopita kwa upande wa mashtaka lakini hadi sasa ni zaidi ya siku 60 wamekuwa wakiahirisha kesi kutokana na shahidi kutokuwepo.

Amedai kuwa kutokana na hatua hiyo wanaiomba mahakama isipokee maombi ya Upande wa Mashtaka ya kuahirisha shauri hilo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kasonde amesema mahakama ilikuwa tayari kusikiliza kwa ushahidi tangu Machi 28, 2019 lakini ilishindikana kutokana kutokana na upande wa mashtaka kutokuwa na mashahidi.

Kasonde alisema Aprili 18, 2019 pia ilitakiwa isikilizwe lakini Upande wa Mashtaka hawakuleta mashahidi.

Kasonde alisema kesi inapoamliwa kwa wakati inamfanya mshtakiwa afanye maendeleo yake ya kiuchumi ili aweze kupata kipato na taifa kwa ujumla

Kutokana na hatua hiyo, anamuachia mshtakiwa ninamwachia huru chini ya kifungu cha 225(5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Mara baada ya Wema kuachiwa muda mchache baadae alijikuta akikamatwa tena na Askari Polisi.

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wake wa Instagram.

MABAUNSA WAWATOA WANAFUNZI WAKIKE KWA NGUVU HOSTEL “ANA VISENTI ANAONEA WATU”

Soma na hizi

Tupia Comments