News Updates

Makamu wa Rais Samia amefanya mazungumzo na Prince William

on

Leo April 17, 2018 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la Buckingham Palace.

Makamu wa Rais  Samia yupo Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola.

Katika mazungumzo yao Makamu wa Rais alimueleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na imekuwa ikichukua hatua za kupambana na kuzuia ujangili ingawa teknolojia bado ni changamoto.

Prince Williams amemuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.

Pia Prince William amemwalika Rais Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi October 2018  jijini London.

MABISHANO MAHAKAMANI MBOWE NA POLISI (April 17 2018)

 

Soma na hizi

Tupia Comments