Leo May 7, 2019 Mtuhumiwa namba tatu katika kesi ya mauaji ya Mwanafunzi wa Shule ya Scolastica Humphrey Makundi, Elima Laban Nabiswa anadaiwa kuishi nchini bila kuwa na kibali kwa zaidi ya miaka sita.
Laban ambaye ni Mwalimu wa Nidhamu katika Shule ya Scolastica anatuhumiwa katika mauji ya mwanafunzi huyo Humfrey Jackson Makundi kushirikiana na mtuhumiwa namba moja Hamis Chacha ambaye ni mlinzi wa shule hiyo na mtuhumiwa namba mbili katika kesi hiyo Edrward Shayo
Wakati wa utetezi wake mshtakiwa namba mbili Labani Nyabiswa pindi alipokuwa anaulizwa maswali na Mwanasheria wa Serikali Mwandamizi Abdalah Chavula amekiri kuwa aliajiriwa kama Mwalimu wa Shule ya Scholastika na hakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini kwa kuwa yeye ni Mkenya na vibali vyake vilikuwa vimeisha muda.
Pamoja na hayo aliyemuajiri Mwalimu huyo ni Edward Shayo ambaye ni mtuhumiwa namba mbili katika kesi ya mauaji ya Mwanafunzi wa Shule ya Scolastica Humphrey Makundi
Imeelezwa kwamba tarehe October, 10.2017 ilikuwa ni tarehe aliyotakiwa kuondoka nchini na kibali hicho kilikuwa cha miezi mitatu kikiwa na jina la Laban Nabiswa nakushindwa kuondoka na kwamba kwa kuishi nchini bila kuwa na kibali ametenda makosa mawili ya kuishi na kufanya kazi bila kibali Wakili Chavula ameeleza
Akitoa ushahidi wake Edward Shayo ambaye ni mtuhumiwa namba mbili katika kesi hiyo baada ya kuulizwa na Wakili wa Serikali Joseph pande amesema ni kweli awali mlinzi huyo Hamis Chacha mshtakiwa namba moja alikuwa mlevi baadaye akampeleka katika hoteli yake na baada ya muda kupita akamrudisha tena katika Shule ya Scolastica kwa ajili ya kuendelea na ulinzi.
Kuhusu taarifa ya kupotea kwa mtoto shahidi huyo alishindwa kutoa majibu huku akitokwa na machozi ndipo Jaji anayesikiliza kesi hiyo Frimin Matogolo kumtaka atulie ajibu maswali anayoulizwa na upande wa mashtaka.
Katika maelezo hayo inadaiwa siku moja baada ya kutokea kwa tukio la mauaji ya Mwanafunzi huyo majira ya saa nne asubuhi Mmiliki wa Shule hiyo inaonyesha Insp. Idd Jumma alimtumia shilingi laki tano nakukiri namba iliyotumika kutuma fedha hizo ni ya kwake. Imedaiwa kwamba
Inspekta Iddi Juma alikuwa Kaimu OCS wa Kituo cha Himo kwa kipindi cha mwaka 2017 ndiye aliyeopoa mwili katika Mto Gona na kuupeleka katika Hospitali ya Mawenzi na sio kwenye Hospitali ya karibu iliopo Marangu na KCMC na kutangaza kuwa mwili waliouopoa ni wa mtu mzima na sio wa mtoto Humfrey Makundi.
Akiulizwa maswali na Wakili Mkuu wa Serikali Joseph Pande amedai kwamba hajawahi kupigwa ili kulazimishwa kutoa taarifa za kuuawa kwa mwanafunzi Humphrey Makundi nakusema alitoa maelezo yake kwa hiari yake.
RAIS MAGUFULI AKIFUTA MACHOZI BAADA YA KUUONA MWILI WA DR. MENGI KWENYE JENEZA