Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Top Stories

Alietengeneza pikipiki aahidi makubwa masomoni “pikipiki naweka pembeni” (+video)

on

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde aliahidi kumsaidia Kijana Zuberi Abdallah Mkazi wa Mkoa Kigoma mwenye umri wa miaka 20 aliyeishia darasa la 6 kuendeleza kipaji chake na kuwatafuta wadau wa kumsaidia.

Kijana Huyo hatimaye amefanikiwa kuanza safari ya ndoto zake, Zuberi alikuwa akijipatia kipato chake kupitia kuwaonyesha watu pikipiki ndogo aliyobuni yenye sifa kama pikipiki kubwa isipokua kubeba mzigo tu.

Kijana Zuberi leo hii ameahidi kuacha kufanya shughuli hizo za kujipatia kipato na kuangalia zaidi masomo yake na Wanafunzi wenzake katika Chuo cha VETA Mkoani Kigoma wamempokea kwa furaha ya hali ya juu na kumpongeza juu ya ubunifu wake.

RAIS WA CHUO AMPOKEA ALIETENGENEZA PIKIPIKI “USITUMIE UMAARUFU”

Soma na hizi

Tupia Comments