Top Stories

IGP Sirro azungumzia ishu ya Mambosasa kuhamishwa DSM

on

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefanya mabadiliko katika baadhi ya mikoa na kuwashusha vyeo baadhi ya watendaji, akiwemo, Kamanda wa Kanda maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo Barnabas Mwakalukwa imesema kuwa siku za hivi karibuni kumeibuka kikundi cha watu wachache kilichoamua kulichafua jeshi kwa kuchapisha taarifa za uongo.

Serikali na vyombo vyake ina utaratibu zake za kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo uhamisho na uteuzi wa maafisa wake“, imesema taarifa hiyo ya Mwakalukwa

BREAKING: MO DEWJI “Nilifungwa kamba, walinibembeleza nile chakula”

Soma na hizi

Tupia Comments