Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Tanzania John Magufuli watazindua kongamano la Kwanza la Kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Rais Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia Septemba 6 na 7, mwaka huu ambapo anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro.
Akizungumzia ufunguzi wa kongamano hilo, Waziri Bashungwa amesema watu 1683 wamejisajili na Watanzania ni 1050, huku matarajio kwa washiriki wa Uganda ni 426.
“Lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wetu tunawasaidia katika mkakati wa kutengeza thamani hapa hapa ili masoko wanayoyapata wapeleke bidhaa zilizosindikwa,” Bashungwa