Top Stories

Mhubiri aliebaka watoto wake ahukumiwa miaka 140 gerezani

on

Mhubiri mmoja nchini Kenya, aliyewabaka watoto wake wawili na kuwapa ujauzito, amehukumiwa kifungo cha miaka 140 gerezani, kufuatia uamuzi wa Jaji wa Mahakama ya Baricho Anthony Mwicigi.

Kulingana na Jaji Mwicigi, mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 51, ambaye pia ni mhubiri katika kanisa moja eneo hilo, alishtakiwa kuwabaka wanawe wawili, kwa sasa wote wana watoto wenye umri wa miezi saba na mwingine ana mtoto wa miezi mitano.

Katika mashtaka yake hayo, mshtakiwa alikiri makosa yake yote mawili, anayodaiwa kuyatenda kati ya Agosti mwaka 2019 na mwaka 2020, katika Kijiji cha Kianyakiru eneo Bunge la Ndia.

Haya yanajiri huku polisi wakianzisha uchunguzi kufuatia kukamatwa kwa mwanaume, anayeshtumiwa kumbaka mwanawe wa miaka mitano hii leo, kuongezea idadi kubwa ya visa vya ubakaji na unyanyasaji dhidi ya watoto ambavyo vinazidi kuripotiwa katika kaunti hiyo.

MWANAFUNZI WA KWANZA KIDATO CHA NNE NCHI NZIMA WASICHANA, MAGUMU ALIYOPITIA, NDOTO ZAKE

Soma na hizi

Tupia Comments