Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Rais Magufuli atema cheche Muhimbili “Tusihukumu sio wote wezi wa mafuta” (+video)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea na kuwapa pole majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini DSM ambao wameungua moto katika ajali iliyotokea jana asubuhi Mjini Morogoro baada ya mafuta yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye lori lililopinduka kulipuka moto. Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 71 mpaka sasa. 

Majeruhi 46 wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbi kwa magari ya wagonjwa na helkopta na majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu Mkoani Morogoro. 

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru na Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura cha hospitali hiyo Dkt. Juma Mfinanga wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wagonjwa 46 waliofikishwa hospitalini hapo ni wale walioungua kwa kiwango kikubwa cha hadi takribani asilimia 100 na kwamba 3 kati yao wamefariki dunia baada ya kufika.

Pamoja na kuwapa pole, Rais Magufuli amewataka Watanzania kutokuwa wepesi wa kuwahukumu kwa madai walikuwa wakiiba mafuta, kwani baadhi yao walikwenda eneo la tukio kwa lengo la kutoa msaada, wengine walikutwa na moto wakiwa katika maeneo yao ya kazi na wengine walikutwa na moto wakiwa wanasafiri katika magari yao.

Rais Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi kubwa wanazozifanya kutoa matibabu kwa majeruhi hao na ameagiza kuwa gharama za matibabu na huduma nyingine kwa majeruhi hao zitatolewa na Serikali.

“Nawashukuru sana Madaktari na Manesi, wanafanya kazi kubwa sana, kweli wanafanya kazi kubwa sana, nimewaona wagonjwa wanahudumiwa vizuri, lakini kikubwa sisi Watanzania tumtangulize Mungu mbele, tuwaombee hawa wagonjwa, lakini na wale waliotangulia mbele za haki nao tuwaombee, na niwaombe ndugu zangu Watanzania katika ajali tusiwe wepesi wa kuhukumu” JPM

“Nimefika humu wodini nimemkuta mmoja ni dereva wa lori la mafuta, alipofika pale aliamua kushuka aende akasaidie, lakini nae ameungua na amelazwa hapa, yupo mwingine alikuwa anasafiri kwenda Mtwara, wala hakwenda kuchukua mafuta, nae ameungua” amesisitiza Rais Magufuli 

WAGONJWA WALIVYOFIKISHWA DSM KWA HELCOPTER KUTOKA MORO

Soma na hizi

Tupia Comments