Top Stories

Goodluck Gozbert, Chris Shalom, Lwanga, Pastor Kuria kufunga mwaka Uwanja wa Taifa kesho

on

Kuna hii good news ya kuifahamu leo December 30, 2018 ni kuhusu Tamasha kubwa la mkesha wa kufunga mwaka 2018 na litakalofanyika December 31  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Staa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Nigeria anayejulikana kwa jina la Chris Shalom, anayetamba na wimbo wake maarufu uitwao ‘My Beautifier’ na nyingine nyingi atakuwepo katika Mkesha huo.

Pamoja na Chris Shalom wengine mbalimbali mahiri kutoka hapa nchini akiwemo Jesica Honore, Goodluck Gosbert, Joel Lwaga na John Lisu.

Muandaaji Prophet Clear Malisa wa Passion Java Ministry, kutoka Ubungo-Kibangu jijini DSM. Waigizaji/wachekeshaji na watu maarufu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa pia kuwepo, akiwemo Pastor Kuria kutoka Show ya Churchchill nchini Kenya.

Katika tamasha hilo hakuna kiingilio na usafiri utatolewa kwa watu wote katika vituo vyote vikubwa vya usafiri Dar es Salaam. Mkesha wa mwaka 2019, umedhaminiwa na Clouds Media Group, Elishadai Shopping Center na Fair Travel Adventures.

MAGUFULI AKISALI “MUNGU MPONYE MAMA YANGU AVUKE 2019” ANAUGUA KIHARUSI

Soma na hizi

Tupia Comments