Top Stories

Trump ampongeza Rais Magufuli kwa kununua ndege Marekani (+video)

on

Tayari ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner (ya pili), imekanyaga ardhi ya Tanzania ikitokea Marekani.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu (Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 262 (22 Biashara na 240 kawaida), ina uwezo wa kusafiri kwa masaa 18 kwa route moja na matenki yake ya mafuta yanachukua hadi Tani 125 kwa wakati mmoja.

“Kuna wengine kila kukicha kazi yao kupiga vijembe vya chinichini, wenye wivu hawakosekani hata ufanye nini, ila tuwaombee kwa Mungu hawa wenye wivu awaondolee wivu wao, na wanatakiwa kujua haya tunafanya kwa uwezo wa Mungu sisi tunatumika kama Wajumbe tu”-JPM

“Mungu anatupenda Tanzania, wee midege kama hii inashuka hapa!, na lazima tujiulize kwanini midege hii haikushuka zamani imesubiri Magufuli awepo ndio ishuke, kwanza nimefurahi sana, Makonda umeomba Hospitali ya Wilaya Ubungo unaomba Billion 1.5 nitazitoa ijengwe Hospitali” – JPM

“Juzi hapa Waziri wetu alipokutana na Trump, Trump ametupongeza kwa kununua ndege Marekani na wakashikana mikono, hii inaonesha tukinunua ndege kwa wakubwa na sisi tunakuwa wakubwa, tunamshukuru Trump na tunamuahidi tutaendelea kununua ndege Marekani,chaguo letu ni Boeing” -JPM

MAAFA: WATU NANE WAFARIKI, 5000 WAKWAMA NJANI, DC KWA UCHUNGU AELEZEA HALI ILIVYO

Soma na hizi

Tupia Comments