Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imemuhukumu Safari Tluway Hangali (29) mkazi wa Kijiji cha Ayasanda Kata ya Bonga Wilaya ya Babati kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 10.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo mnano 19/12/2020 katika Kijiji cha Ayasanda ambapo mtuhumiwa alimpatia mtoto huyo kaisi cha shilingi mia tano(500) na kumpeleka kichakani na kisha kumbaka.
Mwendesha Mashtaka wa kesi hiyo ya jinai namba 16/2021 Grace Mgaya ameiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye kufanya tabia kama hizo.
Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu wa mahakama hiyo ya Wilaya ya Babati Victor Kimario ambapo mtuhumiwa amekiuka kifungu 130(1),(2)(e) 131(1) cha makossa ya jinai sura 16 kilichofanyiwa marejeo 2019.