Tarehe 6 Machi miaka 66 iliyopita, nchi ya Ghana ilifanikiwa kupata uhuru chini ya uongozi wa DaktaKwame Nkurumah.
Ghana ilitumbukia katika makucha ya mkoloni wa Kireno kuanzia karne ya 15.
Baada ya Wareno, Waingereza waliidhibiti na kuikoloni nchi hiyo iliyokuwa mashuhuri kwa jina la “Pwani ya Dhahabu” kutokana na utajiri wake mkubwa wa madini hayo.
Baada ya mazungumzo na Uingereza, hatimaye tarehe 6 Machi 1957 saa sita usiku, Kwame Nkrumah alitangaza Ghana kuwa “huru milele”.
Baada ya uhuru mnamo mwaka 1957 ya Ghana ilikuwa chini ya Kwame Nkrumahambaye alitoa mchango mkubwa katika upatikanaji wa uhuru wa nchi nyingine.
Mwaka 1966 aliangushwa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi wakati alipokuwa ziarani nje ya taifa lake.
Hatua hiyo iliwafanya waghana washerehekee majirani mjini Accra ,wakipasua picha za kiongozi huyo kuanzia maofisini hadi mabango ya barabarani.
Nkurumah alikimbilia uhamishoni nchini Guinea na baadae kufariki huko Bucharest mwaka 1972.