Habari za Mastaa

Ajirekodi video akiimba wimbo mmoja kila siku kwa muda wa miaka 3.

on

dogoMatt Perren kijana mdogo ametumia karibia kila siku kwa muda wa miaka mitatu kujirekodi akiimba wimbo mmoja.

Hivi sasa ameziunganisha hizo video akiimba huo wimbo mmoja kwenye video ya dakika moja na sekunde hamsini.

Kwenye hiyo video anaonekana kuwa na sura ya kitoto hadi sura inabadilika kuwa kijana aliekua.

Video hizi alianza kurekodi January 1 2011 wakati akiwa na miaka 15 na kuziunganisha December 29 akiwa na miaka 18.

Hii ni dedication ya ajabu kurekodi video ya aina moja kwa muda wa miaka mitatu na hivi sasa ikiwa ni siku tano tu tangu aiweke Youtube imeangaliwa na watu zaidi ya milioni moja na laki saba.

Tupia Comments