Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameanza msimu vyema.
Kiungo huyo mshambuliaji alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi wakati Bayer Leverkusen ilipoilaza AC Milan 1-0 kwenye Ligi ya Mabingwa jana usiku.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ana mabao sita na asisti moja katika mechi tisa za mashindano hadi sasa.
BILD inasema kuna vilabu vinne haswa ambavyo vinamtazama Wirtz.
Bayern Munich, Real Madrid, Manchester City na Arsenal wote wanatamani. Barcelona pia wanavutiwa, lakini kutokana na bei ya juu ya €150m, wanaonekana kukosa nafasi.
Paris Saint-Germain wana misuli, lakini hawaonekani kuwa mbioni hivi sasa.
Wirtz ana mkataba na Bayer ambao utaendelea hadi msimu wa joto wa 2027.