Mix

AUDIO: CEO wa Azam FC kuhusu tetesi za kufukuzwa kazi

By

on

Jumanne ya May 30 2017 zilienea stori ambazo hazikuwa zimethibitika kuhusu mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad Kawemba kuwa amefukuzwa kazi ndani ya club hiyo, taarifa hizo zilikuwa zimeenea katika mitandao ya kijamii.

Kupitia Sports Extra ya Clouds FM Saad Kawemba amezungumzia kuhusiana na taarifa za yeye kufukuzwa kazi, zilizokuwa zimeenea toka jana Jumanne ya May 30 2017, ni kweli amefukuzwa kazi?

“Kazi ninayoifanya ni kazi ya wazi kama nilivyoingia ilitangazwa basi nikiondoka itatangazwa lakini jambao ambalo ningependa kuwa watu wafahamu hizi ni kazi za mikataba sio kazi za kudumu kwamba ukiajiliwa ndio basi kwa hiyo mikataba inajadiliwa inafika ukingoni”>>> Kawemba

“Mikataba inajadiliwa inafikia ukingoni kama hamjaelewana maisha yanaendelea mkataba wangu na club unakwenda ukingoni na nafanya mazungumzo na club yangu sasa sijui hizo taarifa zinatoka wapi mimi bado CEO wa Azam FC” >>> Kawemba

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments