Michezo

Nimekusogezea matokeo ya Arsenal vs Newcastle…

on

giroud

Arsenal imefanikiwa kusonga mbele ikiwa ugenini katika ligi kuu ya England baada ya kuichapa mabao 2-1 Newcastle.

Mabao mawili  ya Oliver Giroud katika dakika ya 24 na 28 yalitosha kuipa Arsenal ushindi wa kupiga hatua nyingine mbele.

mou

Moussa Sissoko akiifungia Newcastle goli katika dakika 48 ya mchezo

Kwa upande wa Newcastle bao pekee lilifungwa na Moussa Sissoko kipindi cha pili katika dakika ya 48 ya mchezo.

Ushindi wa Arsenal unakuja ikiwa ni baada ya kutolewa katika klabu Bingwa Ulaya UEFA kwa wastani wa mabao 3-3 dhidi ya Monaco ambapo mchezo wa kwanza walifungwa 3-1 huku mechi ya marudiano walishinda 2-0 na kuifanya Monaco kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments