Michezo

Asmir Begovc awa mrithi wa Peter Cech?, stori iko hapa

on

cech

Ikiwa ni siku kadhaa baada ya klabu Chelsea kumuachia mlinda mlango wao namba moja Peter Cech ajiunge na klabu ya Arsenal, leo hii Chelsea wamethibitisha kumsajili mlinda mlango Asmir Begovic kutokea kutokea katika klabu ya Stoke City.

Chelsea wamemsajili Asmir Begovic (28) kwa mkataba wa miaka minne na ataungana na wachezaji wenzie siku ya jumatano katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza.

asmir-begovic

Begovic atatumia jezi namba moja ambayo ilikuwa ikitumiwa na Peter Cech klabuni hapo. Begovic anatajwa kusajiliwa kwa dau lisilopungua pound million 8.

“Nina furaha kujiunga na Chelsea Fc, baada ya kuzungumza kwa muda mrefu na mwalimu,nafikiri naweza kuendelea nakuwa sehemu muhimu ya timu “  aliandika  Begovic kupitia account yake ya twitter

Hata hivyo Begovic akusita kuishukuru klabu yake ya zamani ya Stoke City

“Ningependa kuishukuru kwa kila kitu klabu ya Stoke City ,mwenyekiti, Mark Hughes, Tony Pulis na mwalimu wa magoalkeeper Andy Quy na wachezaji wenzangu wote bila kusahau mashabiki walionipokea vizuri mimi na familia yangu” aliandika katika account yake ya twitter

begovic

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

 

Tupia Comments