AyoTV

“Hatukutaka kutoa heshima kwa wapinzani wetu” – Kocha Serengeti Boys

on

May 21 2017 imekuwa ni siku ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ( Serengeti Boys ) kuondolewa katika michuano ya AFCON na Niger kwa kufungwa 1-0.

Tanzania ambayo ilikuwa Kundi B na timu za MaliAngola na Niger katika kundi hilo imeondolewa yenyewe na AngolaNiger wameitoa Tanzania kwa kanuni kutokana na timu hizo kufungana kwa point hivyo kanuni ya head to head kwa maana matokeo yao wao kukutana ndio yameiondoa.

Baada ya mchezo kocha msaidizi wa Serengeti Boys Oscar Milambo aliongea na Waandishi wa habari na kueleza anachoamini kimewafanya wapoteze game hiyo, kutolewa katika michuano ya AFCON na kukosa nafasi ya kushiriki kombe la Dunia.

“Kwa bahati mbaya tumeshindwa kufuzu kinyume na matarajio yetu, ilikuwa ni game ambayo tulikuwa na nafasi ambazo tungeweza kuzitumia lakini kingine hatukutaka kutoa heshima kwa wapinzani wetu ilikuwa ni game ambayo tulitaka kushambulia ili tupate goli la mapema tuwe huru lakini bahati haikuwa yetu” – Milambo

Unaweza kutazama video yote ya kocha msaidizi wa Serengeti Boys hapa

Soma na hizi

Tupia Comments