Wakati Serikali ikiendelea kuwataka Wafugaji Wote nchini kutoingiza Mifugo katika Maeneo yote yaliyo hifadhiwa ili kulinda vyanzo vya maji,Hifadhi za misitu pamoja na Wanyamapori, makundi makubwa ya mifugo yameonekana kuvamia kwa kasi bonde la Kilombero yakionekana yakila na kunywa katikati ya ardhi owevu ndani ya bonde hilo, hali ambayo imetajwa kutishia ustawi wa maji yanayo tiririka katika mito inayo jaza Bwawa la Mradi wa umeme wa Nyerere.
Katika hali isiyo ya kawaida camera’ ya kituo hiki imefanikiwa kuyanasa makundi makubwa ya Ngombe yakiwa Katikati ya bonde la Kilombero yakila na kunnywa pasipo shaka yoyote hali Ambayo imetajwa kuathiri shughuli za uhifadhi wa wanyamapori katika eneo hilo.