Michezo

Mikel Arteta aongea kwa mara ya kwanza baada ya kuambukizwa corona

on

Kocha wa Club ya Arsenal ya England Mikel Arteta ameongea na La Sexta kwa mara ya kwanza toka athibitike kuwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID 19).

Arteta ameongea na kueleza hali yake unaendelea vizuri anaamini kuwa ana siku 3 hadi nne za kurejea katika hali yake ya kawaida na mwili kurejesha nguvu.

”Niko vizuri sasa naona nimepona itanichukua siku  tatu hadi nne kuanza kujisikia vizuri kabisa na mwenye nguvu, dalili zinaondoka na ukweli ni kwamba najisikia vizuri”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mike Arteta alibainika au kugundulika kuwa ameambukizwa virusi vya corona baada ya mchezo wa Arsenal wa Europa League dhidi ya Olympiacos.

Soma na hizi

Tupia Comments