Top Stories

Kama ulikuwa humjui Mike Sonko tazama hapa.

on

sonko+gold

Jina la Mbuvi Gidion Kioko Sonko si maarufu sana masikioni mwa watu lakini ukilifupisha na kutaja Mike Sonko hapo watu moja kwa moja watafahamu mtu ambaye unamzungumzia na hii ni kutokana na upekee wa huyu jamaa.

Huyu ni Seneta wa Nairobi ambaye ana muonekano tofauti na muonekano wa wanasiasa wengine ambao wamezoeleka  kupendelea kuonekana nadhifu wakiwa wamevalia suti ambazo ni moja kati ya mavazi ya heshima.

Sonko anapendelea kuvaa kama msanii wa muziki wa Hiphop ambapo hupenda kuvaa vidani vya dhahabu na madini mengine ambayo hung’aa akidhihirisha utajiri alio nao mbele za watu.

Mike Sonko akiwa na wasanii wa muziki wa Injili Size 8 na Rufftone ofisini kwake.

Mike Sonko akiwa na wasanii wa muziki wa Injili Size 8 na Rufftone ofisini kwake.

Hivi karibuni Sonko alitia fora kwenye msiba wa mama mzazi wa Mbunge wa Kamukunji, Simon Mbugua wakati alipoingia na kusababisha watu kuacha kuzungumzia msiba na kuanza kumtazama.

Sonko aliingia akiwa na msafara wa magari ambayo yalijumuisha magari ya kifahari kama SUV na Hummer huku akisindikizwa na ving’ora.

Mike Sonko akiingia kwenye msiba wa mama mzazi wa mbunge wa Kakamega.

Mike Sonko akiingia kwenye msiba wa mama mzazi wa Mbunge wa Kakamega.

Gari ambayo alikuwa amepanda ya SUV ndio iliyotia fora ambapo ilikuwa imenakshiwa kwa dhahabu kwa maana ya gari lote huku akiwa analindwa na askari waliokuwa wamevalia nguo za raia huku wakiwa na silaha.

Sonko aliingia akiwa na wapambe waliokuwa wamevalia fulana zilizoandikwa ‘Team Sonko’ na alidumu kwenye eneo la kutazama mwili wa marehemu kwa dakika mbili baada ya kugundua kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umehamishwa.

Gari aina ya SUV ya dhahabu ikiwa imefunguliwa mlango huku Sonko akiwa na wapambe na walinzi wake

Gari aina ya SUV ya dhahabu ikiwa imefunguliwa mlango huku Sonko akiwa na wapambe na walinzi wake

 Walinzi wa Sonko wakiwa na silaha.

Nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments