Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mike Tyson kwenye headlines, aamua kuimba ‘Hotline Bling’ ya Drake… ilikuwaje? + (Video).

on

Video mpya ya wimbo wa Drake, Hotline Bling umeweka headlines nyingi sana kiasi cha wasanii wengi kuamua kutengeneza remix tofauti ya wimbo huo… Licha ya remix kibao kufanywa na wasanii wengi, watu wengi pia wamekuwa wakitumia  mashairi ya wimbo huo kutengeneza vichekesho vingi na kuvisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na websites pia.

1112

Mike Tyson ni miongoni wa mastaa waliojitokeza siku ya jumanne kwenye kipindi cha ‘The Tonight Show Starring Jimmy Fallon’, kwa ajili ya Interview na kipindi hicho na akiwa kwenye show hiyo staa huyo wa mchezo wa Boxing aliamua kuwachekesha watu baada ya kuamua kutoa style yake ya kuperform single mpya ya Drake, Hotline Bling!

TYSON

Mike Tyson.

Tyson aliwaacha watu wengi hoi baada ya kuimba wimbo huo na sauti yake yenye ‘kithembe’ iliyowafanya watu wengi wacheke sana ambapo kwenye performance yake Tyson alisikika akiimba ‘You uthed to call me on the thell phone…” huku watu wakiangusha kicheko.

Nimekusogezea pia kipande cha video cha Mike Tyson akiwa anatoa burudani ya wimbo huo hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments