Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Stori kubwa kwenye magazeti ya leo June 09 2016 ni kuhusu Bajeti ya mwaka 2016/2017, moja ya stori iliyochomoza ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa”
Serikali imesema kuwa Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza ndiyo mikoa mitano maskini zaidi nchini, aidha mikoa ya Dar es salaam, Kilimajaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini nchini
Waziri wa fedha na mipango Dk Phillip Mpango alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Waziri Mpango alisema tathmini ya hali ya umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za sensa ya watu ya mwaka 2012 na utafiti wa hali ya kipato na matumizi katika kaya wa mwaka 2012,unaonyesha matokeo chanya na kutofautiana kimkoa na wilaya
Waziri Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa 48.9% ukifuatiwa na Geita (43.7%), Kagera (39.3%), Singida (38.2%) na Mwanza (35.3%).
#NIPASHE Serikali imesema Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza ndiyo mikoa maskini zaidi nchini pic.twitter.com/uIOnjAoZaG
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#NIPASHE Deni la Taifa hadi March 2016 limefikia dola bil 20.94 ikilinganishwa na dola bil 19.69 June mwaka jana pic.twitter.com/9Zhswkpxnx
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#NIPASHE Wakati DSM ikiongoza kwa kuwa na viwanda vingi nchini, imeelezwa kuwa 90.4% ya wakazi wake hawana ajira pic.twitter.com/M5S3XC0gdQ
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MWANANCHI Zitto Kabwe amedaiwa kutoa kauli za uchochezi ktk mkutano wake wa hadhara uliofanyika Mbagala DSM pic.twitter.com/Lx9yusrSld
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MWANANCHI Apigwa faini mil 7 baada ya kukiri kumkashifu JPM kwenye facebook, apewa miezi miwili kulipa pic.twitter.com/RwlI9BMEEb
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MWANANCHI Serikali imeikabidhi TRA rungu la kukusanya kodi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kutokusanywa ipasavyo pic.twitter.com/USrNATOTKZ
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MWANANCHI Serikali imeamua kutoongeza kodi na tozo kwenye petrol na dizeli ili kuepuka mfumuko wa bei pic.twitter.com/ZNkpNNpXCo
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MWANANCHI Wanaotaka kusajili namba binafsi za magari sasa mil 10 kutoka mil 5 za awali kwa kipindi cha miaka mitatu pic.twitter.com/V9FC2QDCCL
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MTANZANIA Serikali imetenga bil 2.5 kuwezesha uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi, bil 72.3 kwa ajili ya TAKUKURU pic.twitter.com/KHe9KiVi2L
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#MTANZANIA Serikali kununua ndege tatu mpya na meli moja mpya ktk mipango ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2016/17 pic.twitter.com/5sXX6faDJv
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#JamboLEO PAC imesema imemaliza uchunguzi sakata la Lugumi saa ipo ktk hatua za mwisho kuandaa taarifa yake pic.twitter.com/b9ySiFEfjZ
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#JamboLEO Muhimbili imefanikiwa kukusanya mapato kwa 41% sawa na bil 3.2 kupitia vyanzo vya ndani kwa miezi mitatu pic.twitter.com/CzotGwxuFe
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#RaiaTANZANIA Madereva wawili jela miezi 6 kila mmoja kutokana na kukaidi amri ya kutotumia njia za mabasi ya haraka pic.twitter.com/CJZIZKkZcD
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#NIPASHE Bajeti yajikita kwenye vyanzo vya mapato ya tozo za vinjwaji baridi, vileo, sigara, gesi asilia na mafuta pic.twitter.com/vuYPb3ONqd
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
#NIPASHE Bajeti ya 2016/17 imekata misamaha ya kodi kuanzia kwa taasisi za kidini, wabunge na wawekezaji pic.twitter.com/bFfWtSEJrA
— millardayo (@millardayo) June 9, 2016
ULIKOSA HUU UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 09 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE