fB insta twitter

Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Stori kubwa kwenye magazeti ya leo June 09 2016 ni kuhusu Bajeti ya mwaka 2016/2017, moja ya stori iliyochomoza ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa”

Serikali imesema kuwa Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza ndiyo mikoa mitano maskini zaidi nchini, aidha mikoa ya Dar es salaam, Kilimajaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini nchini

Waziri wa fedha na mipango Dk Phillip Mpango alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Waziri Mpango alisema tathmini ya hali ya umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za sensa ya watu ya mwaka 2012 na utafiti wa hali ya kipato na matumizi katika kaya wa mwaka 2012,unaonyesha matokeo chanya na kutofautiana kimkoa na wilaya

Waziri Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa 48.9% ukifuatiwa na Geita (43.7%), Kagera (39.3%), Singida (38.2%) na Mwanza (35.3%).

ULIKOSA HUU UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 09 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments