Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Milioni 44 fedha ambazo ziliibiwa kwa njia ya mtandao,simu 98 pamoja na Line 51 za Mitandao ya simu.
Katika sakata hili watuhumiwa 21 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo Watuhumiwa nane (8) kati ya hao wamefikishwa Mahakamani na kuhukumiwa vifungo na faini mbalimbali.
“Uchunguzi wa awali umebaini watuhumiwa hawa huwalaghai wananchi kwa kujifanya wao ni watoa huduma za Kampuni za simu kwa kutumia mavazi ya Uwakala wa simu na vitambulisho feki, wengine huwalaghai wananchi kwa kisingizio cha kupata Mikopo nafuu, pembejeo za kilimo pamoja na taarifa za uongo zinazohusiana na ajali, watoto au ndugu wa Karibu kulazwa hospitali, na mtandao huu wa wizi na uhalifu tumeubaini katika kipindi cha Mwezi Desemba 23 mpaka January 24″RPC Katabazi
Aidha Kamanda Katabazi amewataka wananchi kuwa makini na kutoa taarifa Polisi pale wanapomtilia mashaka mtu au kikundi cha watu wanaojifanya watoa huduma za Mawasiliano na kupiga simu TCRA kwa msaada zaidi.