AC Milan wanataka mshambuliaji Olivier Giroud abaki katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu wa joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 37, anakuwa mchezaji huru mwezi Juni atakapomaliza msimu wake wa tatu San Siro.
“Giroud anaendelea vizuri sana, labda ni mapema kidogo lakini sote tunajua uchezaji wake,” msimamizi wa klabu ya AC Milan Giorgio Furlani alisema.
“Ikiwa anataka kubaki Milan, mlango uko wazi.”
Giroud amefunga mabao 12 na kutengeneza mengine tisa katika mechi 29 kwenye mashindano yote akiwa na Rossoneri msimu huu. Amehusishwa na kutaka kutoka kwa vilabu kadhaa vya MLS (tazama sehemu ya Paper Gossip).