Michezo

Rais wa AC Milan ya Italia amesitisha mpango wa kujenga uwanja wa klabu kwa sababu hii….

on

Rais wa klabu ya AC Milan ya Italia Silvio Berlusconi ambaye awali alikubali kuwa katika mipango ya kujenga uwanja mpya wa klabu hiyo na kuachana na mpango wa kuendelea kutumia uwanja wa San Siro. Stori zilizoingia katika headlines hivi karibuni ni kuwa amesitisha mpango wa kujenga uwanja mpya wa klabu hiyo kwani bado wana mapenzi na San Siro.

Silvio-Berlusconi

Awali kulikuwa na stori za klabu hiyo kupewa zawadi ya kujenga uwanja wa klabu yao kati kati ya mji wa Lombardy, mji ambao unatajwa kuwa na idadi ya watu milioni 10. Binti wa Silvio Berlusconi, Barbara alikuwa akiongoza mipango ya ujenzi wa uwanja ambao ungeanza 2018-2019.

download (2)

San Siro

Uwanja huo ambao ungekuwa na uwezo wa kuchukua watu 48000, umetangazwa kusitishwa kwa sababu alizozitaja kuwa bado klabu yake ina furaha kutumia uwanja wa San Siro. Klabu za AC Milan na Inter Milan zote hutumia uwanja wa San Siro kama uwanja wao wa nyumbani ila ukitumiwa na klabu ya Inter Milan kama uwanja wa nyumbani unaitwa jina la Giuseppe Meazza.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments