Mix

Milioni 100 za JayMillions time hii zimemuangukia Mfanyakazi wa Tanesco.

on

Jay Millions 2Tabasamu refu linaendelea kusababishwa na Vodacom kupitia mpango wa Jay Millions ambapo time hii ni zamu ya Irene Mrema wa Dar es salaam aliyejishindia zile milioni 100.

Unaambiwa Irene (hayupo kwenye hizi picha) ni mfanyakazi wa TANESCO ambapo baada ya kujua ameshinda, kwa furaha akasema >>> ”Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni kwa ushindi huu nimeamini kuwa Jaymillions sio promosheni ya mzaha na matangazo bali ya ukweli na nawasihi watanzania wenzangu tuchangamkie fursa hii”

Jay Millions 1

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia) akiwa na afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Jehud Ngolo.

Jaymillions inakaribia kufikia mwisho ambapo mpaka sasa wameshapatikana washindi watatu wa milioni 100/- watano wa milioni 10/-na washindi 40 wa milioni 1/- na maelfu ya wateja wameshajishindia muda wa maongezi.

Washindi wa milioni 100/-ni Uwezo Madegenge wa Kilolo Iringa, Khamis Khalid na Irene Mrema.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, amewahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymiilions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 na njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Tupia Comments