Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa ziadi ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la 43 la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye Chuo cha Sanaa Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Tamasha hilo la siku Nne linatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA amesema kiasi hicho cha fedha kimetoka ndani Ulta Wizara na siyo Serikali kuu.
Kuhusu suala la ubura wa Chuo hicho cha Sanaa Bagamoyo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ametumia nafasi hiyo kwa kuwataka vijana wanaomaliza Elimu ya kidato cha Nnne pamoja na wasanii wafile kwenye Chuo hicho na kupata Elimu ya Sanaa ili waweze kupata cheti kitakachowatambulisha Sanaa yake ndani na nje ya Nchi.
Naye Mkuu wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) Dkt. Harbart Makoye amesema katika Tamasha hilo Nchi mbalimbali zinatarajiwa kushiriki ikiwemo wenyeji Tanzania.
Kuhusu mafunzo, Mkuu huyo wa Chuo hakuwa mbali kuelezea.
Tamasha la sanaa Bagamoyo litakuwa ni Tamasha la siku Nne na litaanza rasmi kesho Oktoba 23 mwaka huu hadi itimisho lake Oktoka 26 mwaka huu na linatarajiwa kufungwa na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Dkt Tulia Jackson.
Mwisho