Top Stories

Milioni 900 zatumika bila kuruhusiwa, malipo hewa Mil. 20, Mkandarasi akimbia (+video)

on

Zaidi ya Milioni 20 za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui zimefanyiwa malipo hewa kwa Wakandarasi wasiofahamika huku Milioni 189 zikitumika bila idhini ya Mkurugenzi na Milioni 900 zikitumika bila kuidhinishwa na bodi na zaidi ya Milioni 100 zikilipwa bila hati ya madai.

Akitoa taarifa kupitia AyoTV na millardayo.com DC Uyui Gift Msuya amesema “Takribani Milioni 20 kazi haijafanyika na mtu aliyepewa tenda haonekani kwa sababu alipewa mtu ambaye hana kampuni wala address, sisi tunawashikilia waliokuwa wamebeba dhamana”.

RC MBEYA AWASAMEHE WALIOSHAMBULIA MSAFARA WA DC, “WALIOPO GEREZANI HATA WAKINYONGWA”

Soma na hizi

Tupia Comments